Burudani

Sababu za Aunty Ezekiel kufika Heaven Sent bila Moses Iyobo (+Video)

Mrs Iyobo kwa sasa Aunty Ezekiel, ameamua kutoa ufafanuzi wa kutinga peke yake katika usiku wa kuitazama filamu mpya ya shoga yake Wema Sepetu iitwayo ‘Heaven Sent’.

Akiongea na Bongo5, mrembo huyo ambaye amejulikana kupitia filamu ameeleza kuwa hakufika na waubani wake, Moses Iyobo kutokana na mtoto wake Cookie kuugua.

“Moses hajaja kwa sababu mtoto alikuwa hayupo sawa, so nikaona sio vizuri wote tukija huku na nikisema mimi nibaki. Wema she is my friend so inakuwa sio vizuri, nikasema wacha mie nije yeye abaki,” amesema mrembo huyo.

Filamu ya Heaven Sent ilizinduliwa kwa mara ya kwanza siku ya Jumamosi na mastaa kibao wahudhuria uzinduzi huo akiwema Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Steve Nyerere.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents