Burudani

Sababu za Bill Nass kutangazaka kuoa, amtaja Alikiba kama mfano bora

Hitmaker wa ngoma ‘Sina Jambo’, Bill Nass amefunguka ni kwanini ameamua kutangaza kuoa.

Bill Nass amesema kuwa anaamua kuoa kutokana anapenda familia, pia wasanii wanatakiwa kuwa kama watu wengine kwani kufanya hivyo haimaanishi msanii atashuka kimuziki.

“Niliposti kuhusu kuoa na pia kuhusu nani nitamuoa nitaamua mimi sio mtu mwingine. Mtu kama Alikiba anaweza kuoa na game yake bado ipo strong kuna kila haja, na pia inatambulisha kwamba ndoa ni jambo muhimu lakini pia sisi ni wasanii na ni watu kama wengine,” Bill Nass ameiambia Wasafi TV.

Ameongeza kuwa pindi alipoenda katika harusi ya Alikiba aliguswa na jinsi mtoto wa muimbaji huyo alivyotaka kusoma dua.

“Mtoto wake alikuwa happy sana kwenye ile harusi kwa hiyo ile ilini-impress zaidi,” amesema.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents