Burudani ya Michezo Live

Sababu za Justin Bieber kufukuzwa gym kisa Taylor Swift zaelezwa

Sababu za Justin Bieber kufukuzwa gym kisa Taylor Swift zaelezwa

Staa wa muziki wa pop nchini Marekani, Justin Bieber, mwishoni mwa wiki iliopita alifukuzwa mazoezini kwenye gym inayojulikana kwa jina la Dogpound, kisa ni ujio wa Taylor Swift.

Inasemakana kuwa, wakati Bieber anaendelea na mazoezi ndani ya gym hiyo ulikuwa ni wakati wa Taylor, hivyo ilikuwa ni lazima aondoke staa huyo aondoke.

Kwa mujibu wa TMZ, Bieber hakutaka kuondoka kwa wakati huo na akawa anajifanya anaendelea kucheza wimbo wake mpya wa Yummy.

Lakini baada ya Taylor kuingia, Bieber hakuwa na sababu ya kuendelea kukaa, aliamua kufuata sheria na kumpisha mrembo huyo kwa kuwa tayari muda wake ulikuwa umemalizika.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW