Sabasaba si mwisho wa maonyesho

7-7_kilimo_kwanaNAJUA watanzania tuna uvivu wa kutembelea sehemu mbalimbali, hususani sehemu ambayo inakuwa maarufu na yenye kuvutia sehemu hiyo ndiyo tunaiona ya hanasa, na  tunaipuuza zaidi kuliko kuipenda kwa madai kwamba ni sehemu ya kuja kupumzika na kutalii wale wenzetu wenye ngozi nyeupe.

 

 

Hii ni kawaida ya watanzania wengi kushindwa kuudhulia sehemu fulani fulani na kuhisi sehemu hiyo ni maaluma na wameumbiwa na Mungu, hao wenzetu lakini si kwa wenyeji.  Kuna vivutio  vingi vipo  Tanzania  pia watu wapo wanaojaribu kuwaelimisha kwamba jamani kutembele, Mbuga za wanyama, Mlima kilimanjaro na hata makumbusho si haramu, ni bei nafuu ni sawa ile unayokunywa bia au kuhonga kwa siku moja lakini bado kazi inakuwa ngumu.

Huwezi amini lakini ni kweli kuna watu wamezaliwa Tanzania, mpaka wanazeeka na kukaribia kufa lakini hawajawahi kutembelea Kivutio chochote hapa, n lakini chaajabu mtu huyo huyo ameshawahi kutembea nchi za nje.

Imefika muda watanzania inabidi tubadilike japo kidogo, ni aibu unapotembelea nchi za mbali na tena za hao ngozi nyeupe, na mwenyeji wako anapofurahia kukuona na akiwa na uhakika umetoka nchi ya maziwa matatu, yenye Mlima kilimanjaro, ndani ya nchi hiyo kuna kila aina ya wanyama poli, waishio kwenye Mbuga maarufu duniani na makumbusho yaliyobeba histori kubwaa lakini kila unapoulizwa swali  unang’ata mdomo yaani hujui kitu.

Haya bwana!! ila kunawengine wanazaliwa mpaka wanatarajia kufa lakini hawajawahi kufika hata Sabasaba, eti ni viwanja vya watoto!! je Ngome Kongwe na Uwanja wa Taifa wa Dar es salaam na Zanzibar je Uliwahi kuingia?
7-7_bunge
Kama hukufanikiwa kwenda Sabasaba mwaka huu basi wacha nikuonyeshe fimbo ya Bunge ‘SIWA’ huenda  mwakani utaenda kuiona Mungu akikujalia uhai.
7-7_chui
Si lazima ukutane naye msituni, ila hata kumuona kwa macho unaweza kujua umbile lake na sio kila siku kwenye video na kuhadithiwa na wasafiri.
7-7_chuii
Huyu hapa analeta raha kumuona katika viwanja vya sabasaba.
7-7_mamba7-7_mayai_ya_mamba

Huwezi amini ila utaamini ukitembelea sehemu kama hizi, yaani hili yai unaweza ukadhani la ndege ama bata mzinga mzee ukalichemsha ukalila, Si vibaya lakini utakuwa umelila hilo dudu linaloonekana kwa nyuma. Yaani hilo ndilo yai la Mamba,  ukubwa wake wote huo lakini anazaliwa kama kuku. Swaali kwako………….  MAMBA  NA YAI NANI WA KWANZA KUZALIWA?
7-7_kenge

Huyu wanamwita Kenge, mtaalamu wa kula mayai ya kuku….. ila sijui kama akiyaona mayai ya Mamba inakuwaje.
7-7_wapelezi

Ukishajijengea mazoea ya kutembelea sehemu kama hizi unaweza kujua maadhi ya majina ni yanani, mimi sikujua kama huyu mdudu mwenye pua kama Nguruwe, umbile kama la Kangarooo kwamba anaitwa Muhanga……. kwa mimi nilijua muhanga ni mtu wa kujitolea kwa jambo fulani (Zaidi kasome kamusi ya kiswahili)
7-7_simba

Habari ya huyu bwana ni kubwa, tena kubwa zaidi kuliko  nilivyokuwa nikifikiria yaani ni mkubwa kimo cha Ng’ombe na ukimuona kalala ujue si mzembe kihivyo.

7-7_ngombe
Huyu pembe zake unaweza ukafikiri ni chuma,
7-7_Habari_leo
kisha nikatembelea sehemu mbalimbali kujionea jinsi makampuni yanavyofanya kazi, nikafika mpaka kwenye kampuni ya TSN wachapishaji wa gazeti la Habari Leo na Daily News hili ni gazeti la Serikali.
7-7_dokta
Nilipoingia kwenye kitengo cha Muhimbili University Of Health and Allied Sciences, hapo nikajionea jinsi binaadam anapoanza maisha yake akiwa tumboni kabla ya kuja kuleta kasheshe duniani.
7-7_kichanga
Hebu fikiria kwanza mara mbili mtoto kama huyu anapokuwa tumboni, kisha fikiria unapoyakatisha maisha yake kabla ya kuzaliwa. Hivi huoni kama ni ukatili wa hari ya juu ambao unapaswa kuulipa….
7-7_mpunga
Haya mambao ya mchina na kilimo kwanza, katuletea magari maalum ya kupandia mpunga….
7-7_upepo

Hili nalo nikasahau sijui gari la nini?, lakini nilipenda kuliona nikajua hata kazi yake itakuwa nzuri kwa mbwembwe zilizowekwa..
HAYA mwenye macho na ameona ila mwenye masikio amesikia amesimuliwa……………. SABASBA SI MWISHO WA MAONYESHO…..tembelea mbuga zetu, ni mali yetu, vimeumbwa kwenye nchi yetu kwajili  yetu…….. By  Mo One’s

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents