Michezo

Sadaka ya noti bandia chupu chupu imponze Mtumishi wa Kanisa la Wasabato

Waumini wa Kanisa la Advestista Wasabato Shinyanga Mjini, wametakiwa wawe wanazikagua fedha zao ambazo huzitoa sadaka  ili kuepuka kumtolea Mungu fedha haramu za noti bandia.

Wito huo umetolewa jana Jumapili Januari 20, 2019, na mweka hazina  wa kanisa hilo, Amosi Magige, wakati wa matangazo ya kanisa, kuwa wiki iliyopita alipokuwa akipeleka fedha za sadaka benki, alikumbana na changamoto ya kuwapo na noti bandia ya Shilingi 10,000.
Magige amesema wakati akiweka fedha hizo benki, ghafla aliambiwa kuwa katika fedha zake hizo kuna pesa bandia noti ya Shilingi 10,000 kitendo ambacho kilimtia wasiwasi kuwa huenda labda ataitiwa polisi na kutiwa nguvuni.
Napenda kutoa tahadhari kwenu waumini wa kanisa hili, pale mnapokuwa mnaleta pesa za sadaka jaribuni kuwa mnazichunguza kwanza kama siyo noti bandia, ili kutuepusha kuingia matatizoni na kama pesa hizi zisingekuwa ni za kanisa sijui ingekuwaje,” amesema Magige na kufafanua.
Baada ya kuambiwa katika fedha za sadaka kuna noti bandia kijasho kilianza kunitoka nikajua basi nimekwisha, lakini mfanyakazi huyo wa benki akaishia kusema tu na huko napo zipo hizi, basi ndio ikawa pona yangu na kuamua kutoa pesa nyingine ili kujazilizia, ambazo zilikuwa za michango mingine,” amesema Magige.
Kwa upande mwingine, Waumini waliitikia wito huo, huku wengine wakidai kuwa hawazijui noti bandia, na kueleza kuwa sio rahisi mtu kwenda kumtolea Mungu sadaka fedha bandia kwa makusudi bali inahitajika  elimu ya kuzitambua.
CHANZO: NIPASHE

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents