Michezo

Sadio Mane aongeza kandarasi Liverpool, Jurgen Klopp amwagia sifa 

Nyota wa klabu ya Liverpool, Sadio Mane amekubali kuongeza mkataba wa kuendelea kusalia ndani ya miamba hiyo ya soka ya England.

Image result for Sadio Mane

Mane mwenye umri wa miaka 26 amekubali kandarasi hiyo itakayo mfanya kuendelea kuwepo Anfield hadi mwaka 2023.

Meneja wa timu hiyo, Jurgen Klopp amemwagia sifa nyota huyo kwakusema kuwa hakuna klabu yoyote barani Ulaya ambayo haitaji aina ya mchezaji kama Sadio.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal amefunga jumla ya mabao 40 kwenye michezo yake 89 aliyocheza Liverpool tangu aliposajiliwa akitokea Southampton kwa dau la pauni milioni 34 mwaka 2016.

Kwa upande wake Mane amesema kuwa hayo yalikuwa maamuzi yake katika fani yake ya soka na anajiskia kuwa mwenye furaha kuendelea kusalia Liverpool.

Huku akiongeza kuwa hiyo ni siku njema kwake na hakuna anachofikiria zaidi ya kuhakikisha anaendelea kuisaidia timu yake ili kuhakikisha itimiza malengo yao hasa ya kutwaa mataji.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents