Michezo

”Sadio Mane ni bora zaidi ya Salah, mbadala wake ndani ya Liverpool ni Mbappe”- Darren Bent

Aliyekuwa Mshambuliaji wa England, Darren Bent ameishauri Liverpool kumuuza nyota wao, Mohamed Salah kama watapata nafasi ya kumnunua mchezaji wa PSG, Kylian Mbappe ama, Jadon Sancho.

Image result for mane and salah who is faster"

Mmisri huyo kwa sasa ndiyo aneye ongoza kwa idadi ya mabao ndani ya Liverpool kwa mashindano yote msimu huu akiwa amejikusanyia jumla ya magoli 18. Akiwa amewasaidia kupata ubingwa wa Champions League na sasa yupo katika mbio za taji la Premier League.

Salah pia ameifungia Liverpool zaidi ya mara tatu kwenye michezo yake miwili ya mwisho, lakini, Bent anaamini Sadio Mane na Roberto Firmino wanathamani kubwa kwa upande wa kocha, Jurgen Klopp.

Darren Bent believes Sadio Mane and Roberto Firmino are more valuable to Liverpool

Bent ameuambia mtandao wa ‘talkSPORT’ kuwa tatizo Mo Salah ni mbinafsi na hiyo ndiyo tafauti yake na nyota hao wengine wawili.

”Ukiangalia uchezaji wake kwa jumla, ukamlinganisha na Mane, naweza kusema Mane ni bora zaidi yake.” – Amesema Bent

”Anaweza kufunga mabao mengi zaidi ya Mane, lakini kiwango cha Mane katika ushiriki wake na timu uwanjani ni kikubwa. Hana ubinafsi yeye huwaangalia wengine kwanza, hivyo huwezi kumuuza Mane ni muhimu sana kwa timu.”

”Firmino, tunafahamu hafungi sana magoli, lakini yeye ndiyo mpishi anaye watengenezea wenzake, kiungo anaye waunganisha wachezaji.”

Mchezaji huyo wa kimataifa wa England, alimalizia kwa kumtaka Klopp kuto kuwa na hofu linapokuja swala la kuuzwa kwa Salah, kama endapo tu anaweza kumleta kikosini Mbappe ama Sancho.

Je msomaji umeupokeaje ushauri wa Darren Bent kwa Liverpool ?

 

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents