Habari

Twanga Pepeta kuzipamba fainali za Safari Lager Nyama Choma Jumapili hii Leaders Club

Kwa mara nyingine tena, Safari Lager inawakaribisha kushuhudia mchuano wa mwisho kuona ni Bar ipi inayochoma nyama bomba zaidi jijini Dar es Salaam, Jumapili hii tarehe 10 March, katika viwanja vya Leaders Club kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 12 jioni

Kutakuwa na bar zilizoingia fainali zikichuana kukupa nyama choma bomba zaidi ambazo ni Fyatamba bar ya – Boko,Soccer City Bar – Sinza,Assenga Pub – Buguruni,Uhakika Pub – Mtoni Kijichi na Titanic Bar – Vingunguti.

Washindi katika shindano ilo watajipatia zawadi zaidi ya shilingi milioni nne na pia watu wanakaribishwa ili waburudike na aina tofauti za nyama choma, kuanzia mapande hadi mishkaki, nyama za Kuku, Ng’ombe na Mbuzi!!.

Chachandu, Kachumbari, Pilipili, ndimu nk..vitakuwepo na pia kutakuwa na zawadi kibao kutoka Safari Lager, huku bendi The African Stars Band, wana Twanga Pepeta wakitarajiwa kutoa burudani ya nguvu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents