Burudani

Safari ya matibabu ya Hawa wa Diamond kwenda India yakwama dakika za mwisho

Msanii Hawa Said maarufu Hawa wa Diamond, amejikuta akirudishwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam (JNIA) baada ya kutotimiza vibali vya kusafiri vya kimatibabu kwenda India.

Akizungumza na MCL Digital baada ya kukwama leo Oktoba 13, 2018 meneja wa Diamond Platinumz ambao ndiyo wamechukua jukumu la kugharamia matibabu hayo, Babu Tale amesema hali hiyo imewakuta wakiwa tayari wameingia ndani ya uwanja wa ndege na kuanza kukaguliwa nyaraka zao mbalimbali.

Babu Tale amesema nyaraka iliyowakwamisha kusafiri ni kibali cha daktari kuelezea hali ya mgonjwa ili wahudumu ndani ya ndege wajue namna watakavyomhudumia.

“Kuna mgonjwa anaweza akawa katika hali ya kuzimia, kutapika anatakiwa ahudumiwe tofauti, hivyo Hawa imeshindikana kwa kuwa hakuna hizo nyaraka inayoonyesha hivyo kutoka kwa daktari na wametwambia turudi itakapokamilika,” amesema.

Hawa, Babu Tale na mama yake, Ndagina Hassan ilikuwa waondoke leo saa 10:45 na ndege ya Shirika la Emirates.

Hawa na mama yake, Ndagina, walifika uwanjani hapo tangu saa 7:00 mchana huku Babu Tale akiwasili saa 9:00 alasiri.

Naye Hawa amewaomba Watanzania kumuombea dua katika matibabu hayo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents