Moto Hauzimwi
Shinda na SIM Account

Safari ya Ndemla Sweden yaota mbawa

Klabu ya soka ya Simba imetoa taarifa ya kusogezwa mbele kwa safari ya mchezaji wao Hamis Said Juma Ndemla iliyopaswa kufanyika leo.

Ndemla ambaye amepata nafasi ya kufanya majaribio ya soka la kulipwa katika klabu ya AFC Eskilstuna nchini Sweden sasa anatarajiwa kusafiri Novemba 9 mwaka huu.

Simba SC yatoa baraka zote kwa Ndemla kutua Sweden

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 

Tunapenda kuwafahamisha kuwa safari ya mchezaji wetu Hamis Said Juma Ndemla iliyokuwa ifanyike leo Jumanne imesogezwa mbele.

Ndemla ambaye amepata nafasi ya kwenda kufanya majaribio katika klabu ya AFC Eskilstuna inayoshiriki ligi kuu nchini Sweden, sasa ataondoka nchini siku ya Alhamis ya tarehe 9 ya mwezi huu.

Mabadiliko haya ya safari hayataathiri muda wake wa majaribio katika klabu hiyo,ambapo atakuwa huko kwa siku 14.

Imetolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano,

Simba Sports Club.

Haji S.Manara.

Leave a comment

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW