Burudani

Safari ya Rayvanny BET yakwiva

Msanii wa muziki wa Bongo Flava Rayvanny kutoka lebo ya WCB, hatimaye safari yake ya kupigiwa kura ili aweze kushinda kwenye tuzo za BET-International imekwiva.

Kupitia ukurasa wa waandaaji wa tuzo hizo, wamepost picha za wasanii wanowania kipengere cha ‘International Viewers Choice Award’ akiwemo Rayvanny tokeya hapa bongo, na kuweka utaratibu mzima wa kuweza kumpigia kura.

Utaratibu huo ni kuandika #Ipickrayvanny,na kuhakikisha kuwa unarepost hiyo hastag iliaweze kushinda kipengere hicho kinachowaniwa na wasanii wengine kama:- Dave (Uingereza), Amanda Black (Afrika Kusini), Changmo (Korea Kusini), Daniel Caesar, Remi na Skip Marley (Jamaica).

Tuzo hizo zinazotarajiwa kufanyika Juni 25 ya mwaka huu katika ukumbi wa Microsoft Theater mjini Los Angeles.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents