Michezo

Sahau kuhusu Simba na Yanga SC, Azam FC hawakamatiki VPL

Ukitoa klabu za Simba na Yanga SC, Klabu ya Azam FC imefanya kweli kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kuongoza Ligi hiyo baada ya ushindi wa bao 2-0 leo Jumapili Januari 21, 2018 dhidi ya Tanzania Prisons.

Kwenye mchezo huo uliopigwa jioni ya leo  kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya mabao ya Azam FC yamefungwa na mshambuliaji Yahya Zayd dakika ya 70 pamoja na Paul Peter dakika ya 82.

Kwa matokeo hayo sasa Azam FC imefikisha alama 30 baada ya michezo 14 na kukaa kileleni ikiizidi Klabu ya Simba yenye alama 29 baada ya mechi 13.

Kwa matokeo hayo, Azam FC itakaa kileleni kwa muda ikisubiri matokeo ya mechi ya kesho Jumatatu kati ya Kagera Sugar dhidi ya Simba SC itakayopigwa kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents