Burudani

Saida Karoli atoa ya moyoni kwa Darassa na Ray C

Msanii mkongwe wa muziki wa asili, Saida Karoli amewamiminia sifa kibao wasanii wa Bongo Fleva, Ray C na Darassa.

Saida Karoli

Saida ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya Orugambo, amesema hit song ya Darassa ‘Muziki’ ni vigumu kuja kushuka na kuwataka wasanii wengine hasa wa hip hop kuchukulia hilo kama somo.

“Wimbo wa Darassa utaendelea kuhit, utaendelea kuwa shule kwa waimbaji wa hip hop. Nitapenda watumie akili alizotumia Darassa, mimi naamini wimbo wa Darassa hauwezi kushuka hata siku moja na Watanzania wengi walikuwa hawapendi muziki wa hip hop lakini Darassa kuonyesha njia kwa sababu sasa hivi hadi kwenye harusi wanaimba acha maneno weka muziki, hadi Bungeni,” Saida ameiambia Clouds FM.

Kwa upande wa Ray C Saida amesema licha ya msanii huyo kupitia matatizo mengi bado uwezo wake upo pale pale na kuna baadhi wamejaribu kumuiga ila wameshindwa.

“Kwa kweli Ray C nampenda sana kutoka moyoni tangu zamani, sauti yake ni nzuri haina mpinzania, wasichana wengi wamejaribu kuiga kuimba kama yeye, wanapenda mvuto wake na muonekano wake lakini wameshindwa,” amesema Saida na kuongeza.

“Na ukiangalia Ray C amepitia matatizo makubwa sana hapa katikati lakini napenda kumshukuru Rais Mstaafu Mheshimiwa Jakaya Kikwete alipomsaidia Ray C, na ningependa Rais wetu wa sasa, Dkt. John Magufuli afanye hivyo ili tuweze kunyanyuka sisi tuliokwama,” ameeleza Saida.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents