Burudani

Sajna awakutanisha Ben Pol na C-Sir Madini kwenye ‘Ningekuwa Single’

Mabibi na mabwana, mko tayari kwa hit single kutoka kwa vijana watatu wenye sauti za hatari? Japo kiukongwe na kiumri hawaendan na na kundi la TGT linaloundwa na Tyrese, Ginuwine na Tank,upamoja wa Sajna, C-Sir Madini na Ben Pol kwenye wimbo mmoja ni kama wanaendana.

Ningekuwa Single

Mwezi ujao vituo vya radio nchini vitashambuliwa na mawimbi ya sauti kutoka kwa hitmaker wa ‘Sitaki Kuumizwa’ na Iveta, Sajna ambaye kwenye wimbo wake ujao ‘Ningekuwa Single’ amewakusanya hitmaker wa ‘Pain Killer’ C-Sir Madini na muimbaji wa ‘Jikubali’ Ben Pol.

Kwa jinsi wimbo ulivyo, Ningekuwa Single utakuwa miongoni mwa zile collaboration chache za waimbaji utakaojadiliwa zaidi. Ni aina ya nyimbo ambazo unaweza kusikiliza siku nzima bila kuuchoka.

Ni kama kila msanii alifungiwa kwenye chumba chake na akapewa beat kuandika vile hisia zake zinamtuma na mwisho wa siku ukizisikiliza verse zao wote watatu, unaweza ukadhani kuwa waliandika kuoneshana nani mjuzi zaidi. Ni kama zile mechi la Wrestlemania za WWE!

Ningekuwa Single uliyotayarishwa na producer Kidboy wa Tetemesha Records unatarajia kuachiwa mwezi ujao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents