AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Sajuki bado anahitaji nguvu zaidi za kifedha

wastaranasajuki
Mwagizaji maarufu nchini Sajuki, hivi sasa yupo katika wakati mgumu kutokana na maradhi anayougua ya  Uvimbe uliokaa tumboni na kumfanya atumie kiasi kikubwa sana cha fedha kwa siku jambo ambalo linafanya kuwa gumu katika kupata fedha hizo.

Mwigizaji huyo ambaye ni mume wa mwigizaji mwenzake Wastara, hivi sasa anajikuta kwa siku akitumia laki mbili hadi laki mbili na nusu katika, hali ya maisha yake kutokana na ugojwa anaougua.

Wasanii waliokaribu na msanii huyo, akiwemo Steven Jacob ‘Jb’ amesema mwigizaji huyo kwa sasa zinahitajika zaidi ya milioni sita ilikuweza kurejesha hari yake katika hari ya kawaida. pia amwigizaji huyo aliweza kufanya mchango siku ya Barthday yake, kwaajili ya kupata fedha ya kumsaidia mwagizaji mwenzake.

Jb amesema katika barthday yake aliweza kukusanaya shilingi milioni moja na laki kama tatu, ambazo ni miongoni mwa ahadi ya shilingi ya milioni tatu na nusu, ambazo wameahidi wasanii wa maigizo.

Jb pia amesema kwamba kwa sasa wasanii ni muda wa kuonyesha ushirikiano ili, kuweza kuboresha na kuunda umoja wa tasnia hiyo.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW