Burudani

Sakata kama la R.Kelly lamuangukia marehemu Michael Jackson, Yadaiwa alimrubuni densa wake

Baada ya dunia kusimama baada ya kampuni ya Lifetime kuonesha filamu ya ‘Surviving R. Kelly’ ambayo imegusa ukweli wa vitendo vya unyanyasaji wa kingono kwa wasichana wadogo, sasa jumba bovu linaenda kumuangukia marehemu Michael Jackson.

Filamu mpya ‘Leaving Neverland’ inatarajiwa kumuacha uchi mfalme huyo wa Pop ikirushwa January 25 mwaka huu. Filamu hiyo imejikita kwenye kuanika vitendo vya ulawiti ambavyo alikuwa akivifanya Michael Jackson kwa wavulana wadogo.

Vijana zaidi ya 30 wametajwa kuzungumza na kuthibitisha kufanyiwa vitendo hivyo, ila ni mmoja ambaye amejitokeza kabla ya kurushwa hewani kwa filamu hiyo: Wade Robson alikuwa mnenguaji wa MJ, amedai kuwa mwimbaji huyo alimlawiti kipindi ana umri wa miaka 7 hadi alipofikisha umri wa miaka 14.

Robson aliwahi kufungua shtaka mwaka 2016 na kuishtaki familia ya Michael Jackson lakini mahakama ilitupilia mbali shauri hilo.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents