Habari

Sakata la kuhama hama vyama, Mbunge mwingine wa CHADEMA kutoa tamko lake leo

Mbunge wa viti maalumu kwa tiketi ya CHADEMA kutoka Mkoa wa Geita, Upendo Peneza leo Desemba 15, 2017, ameitisha mkutano na Waandishi wa Habari, Mkutano ambao umeleta gumzo mitandaoni kutokana na wimbi la Wabunge wa Vyama vya Upinzani kukimbilia CCM.


Mhe. Peneza ameitisha mkutano huo bila kueleza nini hasa anachoenda kuzungumzia kitu ambacho kimeleta maswali mengi kwa wafuasi wa CHADEMA nchini Tanzania.

Mkutano huo unajiri ikiwa ni siku moja tu imepita tangu Mbunge wa jimbo la Siha, Mhe. Godwin Mollel kutoa tamko kuwa amekihama chama hicho na kuhamia CCM.

Soma zaidi-Mbunge wa Chadema ajivua Ubunge, na kuhamia CCM

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents