Habari

Sakata la kutokomeza ushoga Tanzania lilivyoripotiwa na vyombo vya habari vya kimataifa

Baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam kutangaza kampeni ya kutomeza vitendo vya ushoga na usagaji ndani ya jiji la Dar Es Salaam, hatimaye vyombo vya habari vikubwa vya kimataifa vimeripoti tukio hilo kwa mitazamo mbalimbali.

Image result for Tanzania Gay Makonda
RC Makonda

Kituo cha CNN nchini Marekani kimeripoti habari hiyo kwa kuandika “Gavana kutoka Tanzania ametangaza kuwakamata watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja“.

Governor in Tanzania vows mass arrests of LGBT

Gazeti la The Guardian la nchini Uingereza limeripoti kwa kuandika “Mamia ya watu Tanzania wanaishi kwenye taharuki baada ya serikali kuahidi kutangaza majina ya mashoga“.

Thousands ‘living in fear’ after Tanzania calls on public to report gay people

Kituo cha Runinga cha Russia Today cha nchini Urusi nacho kimeripoti kwa kuandika “Tanzania yaunda kamati maalumu ya kukamata mashoga“.

Tanzania launches anti-gay squad to ‘hunt down LGBT community’

Gazeti maarufu la Daily Mail la nchini Uingereza nalo limeripoti kwa kuandika “Tanzania imeunda kikosi maalumu cha kukamata mashoga baada ya Mkuu wa Mkoa kuwataka watu waripoti wanandoa wanaoshiriki mapenzi jinsia moja“.

Tanzania creates hit squad to hunt down gays as governor tells people to report same-sex couples to the police

Gazeti la Financial Times nalo limeandika “Kundi la mashoga Tanzania lipo hatarini kukamatwa“.

Tanzania’s gay community threatened with mass arrest

Gazeti la News24 la Afrika Kusini na Shirika la habari la Uingereza (BBC)  nalo limeandika “Tanzania imetangaza kukamata watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja,”.

Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Jumatano ya wiki hii Oktoba 31, 2018  alitangaza Kamati ya kukamata mashoga, watu wanaorekodi video chafu na makundi ya watu wanaojiuza.

Kwa sheria za Tanzania ni kosa kisheria kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents