Michezo

Sakata la Masoud Djuma lashika kasi, Mhariri amwagia povu Manara ‘Kama atabaki Simba gazeti la Championi ndilo lililomuokoa’

Baada ya Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano ya klabu Simba, Haji Manara kuonyesha kukerwa na taarifa zilizoenea kwenye mitandao kuwa kocha wake msaidizi Masoud Masoud Djuma anatarajia kuondoka ndani ya timu hiyo kwa sababu ya kutofautiana na kocha mkuu Patrick Aussems na kulishutumu gazeti la Championi kuwa ndiyo chanzo cha kuandika habari hiyo aliyoiita ya uwongo, hatimaye Mhariri wake, Saleh Ally amelitolea ufafanu jambo hilo.

Katika mahojiano tofauti yaliyofanywa na kipindi pendwa cha michezo nchini (Sports HQ) kinachorushwa na EF M Radio Msemaji huyo wa Simba alilitaja gazeti hilo na kumtaka Mtangazaji mahiri wa habari za michezo wa siku nyingi, Maulidi Baraka Kitenge kuhoji upande wa pili kuwa taarifa hizo wamezitoa wapi.

Manara afunguka taarifa za kuondoka kocha Masoud Djuma ‘Hakuna atakaekaa Simba’

Kupitia mahojiano hayo Saleh Ally amesema kuwa wao wanavyanzo vingi vya habari kutoka ndani ya klabu ya Simba na wanaushirikiano wakaribu na uongozi wa mabingwa hao wa ligi kuu hata kabla ya uwepo wa Manara huku akisitiza kuwa kama Masoud atakuwa amebaki basi ni gazeti la Championi ndilo lililomuokoa.

”Mara nyingi kunapotokea kunahabari fulani ambayo ina mkanganyiko namna hii ndiyo mara nyingi huwa wanalalamika lakini nikuambie kitu kimoja Simba ni kubwa tuna vyanzo vya habari (source of information) kubwa ndani ya Simba tumekuwa tukishirikiana na Simba hata kabla ya Haji,” amesema Saleh Ally mhariri wa gazeti la Championi.

Ally ameongeza kuwa ”Mimi nimepigiwa simu na viongozi wengi sana wa Simba hakuna anayekanusha hiyo stori wengi wao wanataka kujua tumeitoa wapi na nani aliyesema kwa sababu hiki kitu ndani ya Simba kipo sisi siyo wapuuzi tunajiamini na kazi zetu ambazo tunazifanya kama Haji ambavyo ametumia neno upuuzi.”

”Kwa sababu namjua haji ni mtu ambaye anapenda kukurupukaa, mtu ambaye anapenda kupayukaa lakini mimi nikuambie ninaamini kabisa kama Masoud atakuwa amebaki basi ni gazeti la Championi litakuwa limemuokoa na nimeona gazeti jingine pia limeandika leo.”

”Sasa sidhani watu wote hawa itakuwa sisi hatujui, sema kitu kimoja kwenye sheria za uwandishi wa habari sisi hatuwezi (Disclosure of Sources of Information) kumuweka wazi aliyetoa habari.”

”Kama watu wanakumbuka wasomaji wa magazeti tulimfanyia (interview) mahojiano kocha Pierre Lechantre ambaye ameondoka Simba akazungumza matatizo mengi sana kuhusiana na Masoud na mwisho akaahidi atamuona kocha huyo Patrick Aussems kuzungumza naye kuhusiana na Masoud na matatizo yake.”

”Sasa tunavyanzo vingi na tunajiamini tuwachane na hayo maneno ya haji lakini mimi niseme hivi, sipaswi kuzungumza kama anavyozungumza Haji utafikiri kama wale watu wa mtaani wanao piga piga kelele na wanao payuka, kidogo nataka nijitofautishe na Haji unajua Haji amekuwa si msemaji wa Simba amekuwa msemaji wa Haji FC au Haji Sports Club tupeni muda hili swala mtaona mwisho wake.”

Related Articles

2 Comments

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents