Sakata la Morrison: Simba waitisha kikao, Yanga kukata rufaa Mahakama ya Kimataifa

Mabingwa wa Nchi, Simba SC imetangaza kufanya mkutano na waandishi wa habari hapo kesho siku ya Alhamisi wakati huo huo majirani zao Yanga SC imetangaza kutoridhishwa na maamuzi yaliyofanywa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya shirikisho la soka nchini TFF.

Katika taarifa hiyo Yanga imesema kuwa Uongozi unakusudia kukata RUFAA katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) mara baada ya kupata nakala ya hukumu kutoka Kamati husika.

Hata hivyo Uongozi wa Yanga umewataka wanachama na wapenzi wawe watulivu na kuendelea kushirikiana na Uongozi katika maeneo mbalimbali ya klabu.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW