Michezo

Sakata la Mtibwa Sugar bado kizungumkuti, wakataa kulipa mamilioni ya CAF

Baada ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF  hapo jana kulitolea ufafanuzi sakata la klabu ya Mtibwa Sugar kushiriki michuano ya kombe la Shirikisho na kuitaka kulipa faini ya dola za Kimarekani 1500, timu hiyo imekataa kutoa kiasi hicho cha fedha.

Mtibwa Sugar yakutana na kigingi kizito, yatakiwa kulipa mamilioni kushiriki michuano ya CAF

Akizungumza na radio EFM, Mkurugenzi wa klabu ya Mtibwa Sugar, Jamal Bayser amesema kuwa tayari fedha hizo zilishalipwa kwenye Shirikisho hilo toka wakati huo lilipokuwa likiitwa FAT na hivyo ni wajibu wa TFF kutafuta nyaraka zinazoonyesha malipo hayo.

”Mimi siamini kama CAF hawajui kama hizo fedha zimelipwa au hazijalipwa, sijui hata niseme kitu gani ni taarifa ambazo yani hata ukizisikia hazieleweki,” amesema Bayser.

Bayser ameongeza “Nadhani mpaka tutakapo pata taarifa rasmi ndiyo tutaweza kujua nini tufanye, maana sijajua wanao dai pesa ni TFF au CAF ndiyomaana ni kasema kwamba mpaka nipate taarifa rasmi.”

Mtibwa ambayo itashiriki michuano ya kombe la Shirikisho imesema kuwa haipo tayari kulipa deni hilo mara mbili kama klabu hiyo itashindwa kutekeleza maagizo hayo nafasi kubwa inapewa timu ya Singida United kuiwakilisha nchi kutokana na kushika nafasi ya pili kwenye mashindano ya FA.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents