Michezo

Sakata la Ozil lazua sura mpya: Wakala wa Ozil amkosoa rais wa Bayern Munich

Baada ya kiungo mshambuliaji wa Ujerumani na Arsenal, Mesut Ozil  kutangaza kustaafu timu yake ya taifa ya Ujerumani kwa madai ya ubaguzi wa rangi, mengi yaliibuka lakini kubwa kwa Jumanne hii ni kauli ya wakala wa mchezaji huyo kwa rais wa klabu ya Bayern Munich, Mr Hoeness.

Rais huyo alidai kauli ya Ozil kwamba anabaguliwa sio ya kweli kwani nchi hiyo haijawahi kuwa mambo ya namna hiyo kwenye masuala ya michezo.

Baada ya kauli hiyo, Wakala wa Ozil , Dr Erkut Sogut, amepingana na kauli ya rais huyo huku akidai kwamba alikuwa anatafuta namna ya kulikwepa sakata hilo.

“The comments of Mr Hoeness miss the point completely, as they have absolutely nothing to do with football. He is trying to divert attention away from the real issue, the issue of racism and discrimination in Germany, which is resurging once again within everyday German society,” alisema wakala huyo.

Aliongeza, “If Mesut is such a bad player, what does this say about his opinion on Joachim Low, Arsene Wenger and Jose Mourinho? These are three elite managers who praise Mesut as one of the best in his position. It is laughable that he thinks he is more qualified to judge footballing abilities than these people, with fabricated statistics.,”

Pia wakala huyo amedai kama kweli Ozil sio mchezaji mzuri kama rais huyo wa Bayern Munich alivyodai, je aliwezaji kusajiliwa na Arsène Wenger kukitumikia kikosi cha Arsenal.

By Clinton Abraham Sumari

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents