Tupo Nawe

Sakata la rapper Kodak Black la kumkejeli mpenzi wa Nipsey, Lauren London kuwa ni mjane, limezua sura mpya,baada ya kuibuka na kumuomba msamaha (+ Video)

Baada ya Mambo Kuwa Mazito kuhusu Rapper Kodak Black ameamua Kuomba Msamaha Kwa Kile ambacho wengi Wamekibeba Kama Kumvunjia Heshima Marehemu Nipsey Hussle Kwa Kutoa Kauli Tata kwa Mpenzi wake Lauren London.


Kodak Black imembidi aomba Msamaha huku akijitetea Kwamba Wengi Wamemtafsiri Vibaya na Hana tatizo Lolote na Nipsey Hussle Kwani Anamuombea Akapumzike Mahali Pema na Anaheshimu Mchango wake Kwenye Sanaa.


Huku Akiwataka Mashabiki na Wadau wa Hip Hop Kupunguza Jazba na Kama Wanahisi kasema Kitu ambacho Sio Basi Apate Msamaha Kutoka Kwao.

Ikumbukwe licha ya kodak kuomba msamaha kuna baadhi ya wasanii walimtaka aache kuropoka na badala yake aitake familia ya nipsey na Lauren msamaha.

TI alimuomba Sana Kodack Black Kutengua Kauli Yake na Hana Utani Katika Hilo Kwa Kuwa Nipsey Hussle Alikua ni Rapper Anayemkubali.

Lakini Kodakl Black alisikika Katika Video Hii ambayo alikuwa Insta Live Akimuongelea Vibaya Mpenzi wa Rapper Nipsey Hussle amabye ni mwanadada Laurent London

Kwenye Kipande Hiki Ambacho Wengi Wamekikata na Kuwa Gumzo zaidi Kwenye Mitandao Kodack Black alikuwa akisikika Akisema Kuwa Kwa Sasa Mwanadada Lauren London ni Mjane na Anaweza Akampa Hata Mwaka Mzima Awe Nae Kwa Ajili ya Kumpa Furaha Kwa Kuwa Anampemda.

Hii Imeleta Mijadala Mingi Sana Mitandaoni na Mastaa Tofauti Wakijirecord Kumtaka Afute Kauli Yake Kabla Hawajafanya Maamuzi Magumu Juu Yake Kuhusu Maisha ya Npsey na Lauren London.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW