Habari

Sakata la ziwa Nyasa: Waziri Membe akutana na wananchi wa Mbamba Bay

That’s why we love social media! Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Bernard Membe weekend hii amekutana na wananchi wa
MBamba Bay, Mbinga, mkoani Ruvuma.

Cha kufurahisha ni kwamba Mheshimiwa Membe yupo active kwenye mtandao wa Twitter na hivyo baada ya mkutano huo alikuwa busy kuweka picha na maelezo ya kile kilichoendelea kwenye mkutano huo na hivyo kuonesha namna mitandao ya kijamii ilivyo sehemu muhimu katika maisha ya sasa.

Huna haja ya kusubiri habari za TV za usiku ili ufahamu kilichoendelea, haya ni maelezo aliyokuwa akiyatweet yanatoa picha ya mkutano wake.

Mkutano wangu wa kwanza na Wazee wa Mbamba Bay unaofanyika pwani ya Ziwa Nyasa. Niko pamoja na Mbunge wa Mbinga na DC.

Nimekutana na Mzee Ndembeka, ana miaka 85,amezaliwa Mbamba Bay, Babu yake aliishi hapa na kuwa Chief mwaka 1885.

Mzee Ndembeka ana hazina kubwa sana ya historia, amenikabidhi vitabu na ramani vyenye ushahidi, anasema mpaka uko katikati.

Mzee Ndembeka hatambui Ziwa Malawi, analijua Ziwa Nyasa tu(kwa lugha ya chechewa,ndio amekuwa akivua samaki na kutumia maji yake wakati wote.

Wenyeji wanasema wanavyo viashiria vya mpaka katika Ziwa Nyasa, wavuvi wamekuwa wakiheshimu viashiria hivyo vya asili ikiwemo safu za milima.

Kwa mujibu wao, mipaka yao ya asili wamekuwa wakiiheshimu sana, na wavuvi wamekuwa hawaingiliani wala hawana migogoro.

Prof. Kabisama, mzaliwa wa Mbamba Bay, miaka 77 anasema tatizo letu tunaegemea sana kwenye vitabu vya Oxford vilivyoandikwa na watu baki.

Wazee wanasema meli za Malawi ikiwemo MV. Ilala na Mtendele zinashusha na kupandisha bendera zinapopita katikati ya Ziwa Nyasa.

Mvuvi hapa ananiambia kuwa wao wenyewe wakifika katikati kuna mkondo wa maji unaotenganisha mawimbi, wao kiuvuvi wanatumia kama mpaka.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents