Michezo

Salah, Mane, Emre Can wawasili Merseyside wakitokea falme za kiarabu (+Picha)

Kikosi kizima cha Liverpool kimetua salama katika mji wa Merseyside uliyopo kaskazini magharibi mwa England kikitokea katika Falme zakiarabu, Dubai ambako kilikuwa katika maandalizi ya msimu huku kikiwa na wachezaji wake mashuhuri Salah, Mane na Emre Can.

Wachezaji wa kikosi cha Liverpool, Sadio Mane,  Salah, Emre Can na wengine wakiwasili England wakitokea Dubai ambako walikuwa katika maandalizi ya msimu 

Kocha, Jurgen Klopp ametua Merseyside ambapo mndipo makao makuu ya klabu hiyo yalipo pasipo Mbrazili Philippe Coutinho ambaye amesajiliwa kwa dau nono la paundi milioni 145 kwenda Barcelona.

Kocha wazamani wa Liverpool, Brendan Rodgers ambaye kwa sasa anafundisha timu ya Celtic ndiye aliyemleta Coutinho  akitokea Inter Milan mwaka 2013.

Rodgers anaamini Barcelona imepata mchezaji bora zaidi kwa wakati huu.

“Wakati tunamchukua na kumIeta hapa hakuwa na utimamu wa mwili wa kushindana katika ligi ya England  kwakuwa alikuwa kijana mdogo lakini alikuwa akionekana kuwa bora,” amesema kocha Rodgers.

Rodgers ameongeza “Tulitoa paundi milioni 8.5 kwaajili ya kumnunua na alinitumia ujumbe mfupi wakati akiwasili Barcelona, nikijana mzuri ambaye hakuwahi kuwa na matatizo na mimi.”

 

 

 

Beki wa Liverpool,  Joe Gomez akiwasili

Mchezaji, Sadio Mane akitua Liverpool

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents