Michezo

Salah siyo mtu mzuri hata kidogo kwa rekodi hii Ballon d’Or itamuhusu 

Siku chache tu kupita tangu kutajwa kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa kulipwa wa mwaka 2018 nchini Uingereza, Mohamed Salah amezidi kuimarisha utawala wake wa soka barani Ulaya baada ya hapo jana kuisaidia timu yake ya Liverpool kuchomoza na ushindi wa jumla ya mabao 5 -2 dhidi ya AS Roma klabu bingwa barani Ulaya.

Baada ya kuifungia jumla ya mabao 2 timu yake ya Liverpool na kuchangia pasi mbili za mwisho zilizo changia magoli ‘assist’ hapo jana kwenye dimba la Anfield, mshambuliaji wazamani wa klabu hiyo, Robbie Fowler amesema kuwa Mohamed Salah si mtu wa kawaida na anastahili kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia, Ballon d’Or.

UEFA: Mo Salah, Mane na Firmino wapeleka kilio Italia

Kupitia mahojiano yake na BBC Radio 5, Robbie Fowler ambaye amewahi kutajwa kwenye tuzo hizo mwaka 1996 amesema kiwango kinacho onyeshwa na Salah ni dhahiri anastahili tuzo hiyo na mchezaji huyo siyo mtu wa kawaida hata kidogo kama watu wanavyomchukulia.

Salah siyo mtu wakawaida hatakidogo kama watu wanavyomchukulia, kwa namna stahili ya uchezaji wake na ufungaji wake mabao ni mchezaji mwingine.

Mtu ambaye tumemzungumzia hata kabla ya mchezo na anachofanya ndani hakika huyu ni wasayari nyingine.

Tutarajie makubwa yanakuja kutoka kwake kama Liverpool itafanikiwa kuimaliza Roma na kutinga hatua ya fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.

Mo Salah ashinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka PFA, Sane afanya kweli

Salah mpaka sasa amefunga jumla ya mabao 43 kwenye michezo 47 aliyoingia uwanjani msimu huu rekodi ambayo unamuweka kwenye sayari ya moja na wachezaji, Lionel Messi, Cristiano Ronaldo na Neymar.

  • Salah anakuwa Mwafrika wa kwanza kwenye historia ya soka kufunga angalau magoli tisa kwenye michuano ya European Cup/Champions League kwa msimu mmoja.
  • Amefunga amefanikiwa kufunga bao kwenye kila mchezo mmoja kwa michezo ya mitano ya Champions League – ni mchezaji pekee wa Liver kufunga mabao matano kwa mfululizo kabla ya kukutana na Roma kisha Steven Gerrard kati ya Octoba 2007 na Februari 2008.
  • Salah amefunga jumla ya mabao 10 kwenye michuano ya Champions League msimu huu.
  • Mmisiri huyo anakuwa mchezaji wa tano kutoka Ligi ya Uingereza kufunga zaidi ya mabao 40 kwa msimu mmoja (31 mabao, pasi zilizo changia goli ‘assists; nane). Alan Shearer (47 mabao mwaka 1994-95), Andrew Cole (47 mabao, mwaka 1993-94), Thierry Henry (44 mabao, mwaka 2002-03) na Luis Suarez (43 mabao, mwaka  2013-14).
Bila shaka kiatu cha dhabu msimu huu huwanda kikatua Afrika – Mohamed Salah ambaye mpaka ana magoli 28, rekodi ya magoli mengi kwenye msimu wa EPL ni magoli 31 (Shearer, Ronaldo na Suarez) – Rekodi ya magoli mengi katika mashindano yote ni kwa wachezaji wa EPL ni magoli 42 aliyoweka Cristiano Ronaldo 2008 – mpaka sasa Salah ana magoli 36.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents