Burudani

Salama Jabir na utani wa Kiswahili kwa Kanye West! Very funny!!

sal kanye

Kama Kanye West angekuwa anaelewa Kiswahili huenda angefanya kila awezalo ili aonane na mtangazaji wa kipindi cha Mkasi, Salama Jabir. Huenda pia Kanye ni miongoni mwa wasanii wa Marekani wanaomvutia Salama na kama angekuwa karibu angemtafuta kwa show ya Mkasi. Tunajiuliza angemuuliza maswali gani!! Maswali ya haraka haraka ambayo tunadhani Salama angemuuliza Kanye ni kwa mfano ‘Ni kweli uliangalia sex tape ya Kim na Ray J’!!

So hivi karibuni kupitia Twitter Salama amekuwa akimwandikia Kanye (kwa utani) mambo kibao kwa Kiswahili na kama ukisoma anayomwambia huenda ukakaribisha tabasamu usoni mwako ama kicheko kirefu. Bahati mbaya hajawahi kujibu.

Hizi ni baadhi ya tweets alizomwandikia Kanyewest:

Umesahau Kufunga Zipu Blaza…Ya Begi Lakooo… @kanyewest

Oooooi… Umelala Mdomo Wazi… @kanyewest

@kanyewest Unaweza fanya mpango ukatusapraizi na mvua huku?!

Kesho Ntakuambia Maana Ya Jina Lako Kwa Lugha Yangu… @kanyewest

Mshipi Wako Umevua Kitu?! Kitoweo Cha Familia Baba..Mama’ako Angekua Proud…Saaaana!! Amlaze Pema Jalali. @kanyewest
Unaangaliaga Pilau?! @kanyewest

Ushawahi kula kipilaaa?! @kanyewest

Bi Kidude Akikuuuona Tu Atakuambia “Mume Wangu Ulikua Waaapi?!” @kanyewest

Bi Kidude?! Kama Humjui Huyu Utakua Umefeli…Maana Unahitaji Kolabo Kwasababu Za Kibiashara… @kanyewest

Wakati Wa OPP Nlikua Kwetu Tanga…Nasoma Bombo Praimari…Wewe Je?! @kanyewest

Unaangalia Mechi?! @kanyewest Au Ushauza?!

Mwanangu Nna Mwanangu Kaaaaaama Weeeeewe… Kosa La Marehemu Baba! @kanyewest

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents