Burudani

Salma Mahin na Linias Mhaya: Washiriki wa BSS wenye historia za kuvutia

Shindano la Bongo Star Search lipo kwenye hatua ya top 20. Kwenye kipindi cha jana usiku kupitia ITV, washiriki hao walikuwa wakitoa historia zao, wasanii wanaowavutia, nini wanatarajia kufanya kwenye shindano hilo na mambo mengine.

Pamoja na washiriki wengi kuwa na historia nzuri, washiriki wawili walitoa historia zilizovutia zaidi.

Linias Mhaya

Ni mshiriki anayefahamika kwa muonekano wake wa nywele. Akiwa anaiwakilisha Mwanza, mshiriki huyo aliiwakilisha Tanzania kwenye shindano la mwaka huu la Tusker Project Fame lakini hata hivyo alitolewa katika hatua za mwanzo kabisa. Hakukata tamaa na hivyo aliamua kujaribu bahati yake kwenye Bongo Star Search. Linias ni mhitimu wa chuo kikuu aliyeamua kufungua kijiwe cha kuuza chips baada ya kutafuta kazi bila mafanikio.

Salma Mahin


Muonekano wa kihindi wa Salma unawafanya watamazaji wadhani huenda mrembo huyo amepotea njia kwakuwa anaonekana ametoka kwenye familia bora (japo inaweza isiwe hivyo). Akizungumza Kiswahili kizuri, Salma ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha nne haoneshi dalili zozote kuwa amekwenda kwenye shindano hilo kuuza sura bali kukiwania kitita cha shilingi milioni 50 kama washiriki wengine.

Wazazi wake walitengana wakati yeye akiwa na umri mdogo japo kila mzazi amekuwa akihusika katika kumlea kwa namna yake. Hakushiriki BSS kirahisi kwakuwa baba yake hapendi kabisa mwanae ajihusishe na muziki. Kikubwa ni support anayoipata kutoka kwa mama yake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents