Bongo Movie

Salma ‘Nisha’ Jabu asema soko la filamu mwaka 2013 lilienda mrama

Muigizaji wa filamu Salma Jabu aka Nisha amesema kutokana na takwimu za mauzo ya filamu nchini soko la filamu za kibongo limeshuka huku akiwataka wasanii kuwa wabunifu ili kuongeza ubora katika filamu zao.

nishamsanii

“Katika filamu sasa hivi mambo mengi yameongezeka inabidi wasanii tukaze zaidi ili tusiweze kushuka kisanaa ili soko letu lisishuke,” Nisha ameiambia Bongo5. “Kwa takwimu ya mwaka uliyopita ni kwamba kidogo tumeshuka, sasa inabidi tufanye kazi kwa bidii kuongeza ujuzi,kuongeza akili,kuongeza maarifa,kujituma zaidi,kubuni vitu vingine ambavyo watu hawakuwaHi kufanya na kujipanua iimataifa zaidi, tofauti na kufanya kazi ambazo ni ni zilezile ambazo wanafanya Watanzania.”

Wakati huo huo Nisha amewataka Watanzania kukaa mkao wa kula ambapo mwaka huu ataachia filamu yake iitwayo ‘Gumzo’ aliyoigiza na Wastara, King Majuto na Hemedy na kwamba baada ya hapo ataachia filamu aliyocheza na mrembo wa video za muziki, Agnes Masogange na Joti.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents