DStv Inogilee!

Salum Mkemi aandika ujumbe mzito kabla mechi ya Simba vs Mbabane Swallows ‘Usiku wa deni haukawii’

Aliyekuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga, Salum Mkemi kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram ameandika ujumbe wenye kuonyesha kutowaunga mkono watani zao Simba hii leo ambao watakuwa na kibarua cha kupigania pointi tatu dhidi ya Mbabane Swallows katika dimba la Taifa.

Mkemi ameandika ujumbe huo ambao umeonyesha kutomuunga mkono mtani wake Simba kutokana na maneno hayo kusomeka kuwa watafanya kama vile walivyofanyiwa.

”Kama mlivyotufanyia ndivyo tutawafanyia USIKU WA DENI HAUKAWII KUCHWA,” ameandika mjumbe huyo wa zamani wa kamati ya utendaji wa Yanga, Salum Mkemi.

Hata hivyo ujumbe huo umepokewa na hisia mbalimbali kutoka kwa mashabiki wa pande zote mbili kwenye mtandao wa huo wa Instagram.

maarufu_yasini

Kilichokukimbiza yanga unakijua

shoubille

Al-Kisas Hakii

iamalifedha

uzalendo kwa wenye uzalendo sio kwa kila MTU, karibu umuone triple C uzalendo tuachie sisi Simba

florentinwilliam

Tunashukuru umechangia mapato

tashman493

Njooni kwa wingi vyura nyie

geofkiswaga

@omary_wabongo_gabon hahahahaahaa. Uzalendo mwisho Tazara

kush.diet

As long as umenunua ticket @mkemi_le_champion be our Guest broh.😂😂

jonathanjaphet_

Si tunashukuru kwa kutuongezea mapato tena kwa tiketi yako ya vip☺☺

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW