Michezo

Samatta aipatia ushindi KRC Genk

Usiku wa Mei 7, 2017 mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta aliifungia timu yake ya Genk goli moja na kuisaidia kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya AS Eupen katika mechi ya play off ya ligi ya Ubelgiji.

Samatta alichangia goli la kwanza kwa kutoa pasi ya mwisho iliyosababisha kufungwa kwa goli hilo na Jere Uronen dakika ya 18 kipindi cha kwanza. Samatta alipiga shuti kali ambalo lilimgonga beki kisha kumkuta Uronen ambaye aliukwamisha mpira kambani.

Nahodha wa Tanzania Mbwana Samatta akafunga bao la pili dakika ya 28 akimalizia kazi nzuri iliyifanywa na Thomas Buffel na kuipa Genk uongozi wa 2-0.

Eupen walipata goli lao pekee dakika ya 76 kupitia kwa H.C. Onyekuru na kupelekea mchezo kumalizika kwa Genk kuibuka washindi wa mchezo kwa magoli 2-1.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents