Burudani ya Michezo Live

Samatta aisaidia timu yake ya Genk kutwaa ubingwa wa Ubelgiji, awa kinara wa ufungaji, wachezaji wenzake wamuimbia nyimbo hii (+ Video)

Samatta aisaidia timu yake ya Genk kutwaa ubingwa wa Ubelgiji, awa kinara wa ufungaji, wachezaji wenzake wamuimbia nyimbo hii (+ Video)

Mshambuliaji wa Taifa Stars  na Klabu ya Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta ameisaidia klabu yake ya Genk kutwaa ubingwa wa Ubelgiji. katika mchezo wa mwisho baada ya sare ya 1-1 ya KRC Genk dhidi ya Anderlecht na kipigo cha Club Brugge cha 2-0 kutoka Standard de Liege KRC Genk wanatangazwa kuwa Mabingwa wa Ligi Kuu Ubelgiji 2018/2019 wakiwa na mchezo mmoja mkononi.

Msimamo wa ligi uko hivi:-

Hawa ndio wafungaji bora wa ligi hiyo Samatta akiwa kinara wa ufungaji:-

Ubingwa huo umewapa KRC Genk nafasi ya kucheza UEFA Champions League hatua ya Makundi moja kwa moja msimu wa 2019/2020. Baada ya ushindi huo Wachezaji wenzake wa wa KRC Genk wakiwa dressing room baada ya kutangazwa Mabingwa wa Jupiler Pro League 2018/2019.

Baada ya kutangazwa Mabingwa KRC Genk walitembea katika bus la wazi na bus hilo likiwa na wachezaji na benchi la ufundi na baada ya kumaliza Party ilifanyika Limburghal saa 22:00 shabiki wa kawaida walilipia Euro 10 (Tsh 25,695).

Na wakati wa sherehe hizo Shabiki mmoja akiwa na bendera ya Tanzania katikati ya mashabiki wa Genk wakishangilia ubingwa.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW