Michezo

Samatta asubiri vibali vya kazi Tu, Man City yangojea ofa ya PSG kwa Guardiola na Mourinho kushusha kifaa kipya Spurs, wengine sokoni

Kocha wa klabu ya Aston Villa amesema kuwa Mshambuliaji wa Tanzania na klabu ya KRC Genk, Mbwana Samatta anakaribia kuitumikia timu hiyo inayoshiriki ligi kuu England

Mbwana Samatta

Mbwana Samatta amefungia Genk mabao 43 katika ligi ya Ubelgiji

Dean Smith alizungumzia usajili huo wa Samataa mara baada ya kupata matokeo ya sare ya mabao 1 – 1 dhidi ya Brighton mchezo wa ligi kuu England uliyopigwa hapo jana usiku.

Kwa mujibu wa mtandao wa Birmingham Mail, Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27, tayari ameshafanyiwa vipimo vya afya na kinachosubiriwa mpaka sasa ni kukamilika kwa vibali vya kufanya kazi.

Everton inajiandaa kuwasilisha dau la £30m kumnunua kiungo wa kati wa Juventus Mjerumani Emre Can, ambaye mkataba wa sasa umekamilika. (Sunday Mirror)

Emre Can

Liverpool itamenyana na Chelsea kumsaka mshambuliaji wa RB Leipzig na Ujerumani Timo Werner,23. (Sunday Mirror).

Mkufunzi wa Paris St-Germain Thomas Tuchel, amesema klabu hiyo bado inamhitaji beki Layvin Kurzawa. Kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa wa miaka 27-ananyatiwa na Arsenal.(Goal)

Manchester City wanajiandaa kupokea ofa ya PSG ya kumnunua Pep Guardiola, ikiwa klabu hiyo ya Ligue 1 itamtimua Tuchel. (Sunday Express)

Layvin Kurzawa

Paris St-Germain Thomas bado inataka huduma ya beki wake Layvin Kurzawa

Manchester United imeshindwa na Real Madrid katika kinyang’anyiro cha kumsajili kiungo wa kati wa Ajax na Uholanzi Donny van de Beek, 22. (Daily Star Sunday)

Mkurugenzi wa kiufundi wa Arsenal, Edu amekutana na wawakilishi wa kiungo wa kati ma mlizi wa Athletico Paranaense, Bruno Guimaraes kuhusiana na uwezekano wa kununua kwa kiasi hadi cha euro milioni 30 sawa na (£25.6m) kumpata mchezaji huyo wa Brazili wa miaka 22. (Goal – in Portuguese)

PSG iko tayari kumpatia ofa ya mkataba wa thamani ya euro milioni 12 kwa mwaka, kiungo wa kimataifa wa Senegal Kalidou Koulibaly, 28, akikubali kuondoka Napoli. (Foot Mercato – in French)Senegal Kalidou Koulibaly

PSG itafanikiwa kumnyakua Senegal Kalidou Koulibaly kutoka Napoli?

Kalabu ya Roma ya Italia inataka kumsaini winga wa zamani wa Manchester United Adnan Januzaj kwa mkopo kutoka Real Sociedad, kwa lengo la kumnunua kiungo huyo wa kimataifa wa Ubelgiji msimu wa joto. (Mail on Sunday)

Mkufunzi wa Tottenham Hotspur boss Jose Mourinho ana matumaini ya kumsajili mshambuliaji mwezi huu wa Januari, baada ya kukosa huduma ya Harry Kane ambaye anauguza jeraha kwa hadi miezi mitatu. (Evening Standard)

Mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani, 32, ataomba Paris St-Germain isimshirikishe katika mechi ya Jumapili dhidi ya Lorient ili kushinikiza uhamisho wa kwenda Atletico Madrid. (Marca)Edinson Cavani

Edinson Cavani anataka kuhamia Atletico Madrid

Newcastle United wanakaribia kumsaini kwa mkopo winga wa Austria Valentino Lazaro, 23, kutoka Inter Milan, wakitarajia kumnunua kwa 20m euro (£17m). (Tuttomercatoweb – in Italian)

Real Madrid imepuuzilia mbali ofa ya kutaka kumsajili kwa mkopo James Rodriguez,28, na wako tayari kumuuza kiungo huyo wa kati wa kimataifa wa Colombia. (Marca)

Atletico huenda ikamnunua Alexandre Lacazette, 28, wa Arsenal au Paco Alcacer, 26, wa Borussia Dortmund ikishindwa kumsajili Cavani. (Mundo Deportivo – in Spanish)Alexandre Lacazette

Atletico huenda ikamnunua Alexandre Lacazette(kulia) kutoka Arsenal

Juventus imewasilisha ofa ya kumuuza kiungo wa kati wa Italia Federico Bernardeschi, 25, kwa Barcelona kama sehemu ya makubaliano ya kumpata kiungo wa kati wa Croatia Ivan Rakitic, 31. (AS)

Kiungo wa kati wa Flamengo Reinier Jesus, 17, amekutana na wawakilishi wa Real Madrid kukamilisha mpango wa uhamisho wake. (AS)

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents