Michezo

Samatta auliza swali gumu na kuanzisha mjadala mtandaoni, hiki ndicho anachokitamani lakini hakiwezekani

Mshambuliaji wa Tanzania na klabu ya KRC Geng, Mbwana Samatta ameanzisha mjadala kwenye akaunti yake ya kijamii ya Instagram huku akionyesha hisia zake za kutamani kutua katika soka la barani Ulaya kabla ya kufikisha umri wa miaka 18.

Image result for samatta

Samatta ameandika ujumbe huo huku akiomba watu kuchangia baada ya kuuliza swali kuwa ni jambo gani mtu unatamani likutokee mapema kwenye maisha yako.

”Tujadili kidogo. Ni jambo gani unatamani lingetokea katika maisha yako mapema?🤷‍♂️ . Mimi natamani ningekuwa katika soka la ulaya kabla ata sijafika 18.  Nb.hatukosoi mipango ya mungu.” Ameandika Mbwana Samatta.

Samatta ameanza kulitumikia soka la Ulay akiwa ameshavuka miaka 18 tayari, huwenda ikawa ndiyo sababu ya yeye kutamani kucheza wakati kabla hata kufikisha umri huo kitu ambacho hakiwezekani tena.

Nahodha huyo wa Taifa Stars, Mbwana Ally Samatta alijiunga na KRC Genk akitokea katika klabu ya TP Mazembe mnamo Januari 2016 kwa kandarasi ya ambayo ingemuweka ndani ya miamba hiyo ya soka ya Ubelgiji hadi msimu wa mwaka 2019/20.

Mshambuliaji huyo ambaye amepata kuitumikia Simba SC msimu wa mwaka 2010/11 kabla kutimkia TP Mazembe kutokea Lubumbashi nchini Congo ni mzaliwa wa mwezi Desemba mwaka 1992 mpaka sasa akiwa na umir wa miaka 26 huku akiwa Mtanzania wa Kwanza kupata kucheza michuano ya UEFA Champions League.

https://www.instagram.com/p/B2lyEh6oqm8/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents