Michezo

Samatta awa mfungaji bora, TP Mazembe yachukua ubingwa wa Afrika

Klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo imechukua kombe la michuano ya mabingwa wa Afrika baada ya kuifunga mabao 2-0 USM Alger ya Algeria kwenye fainali zilizochezwa jana mjini Lubumbashi.

Mbwana
Samatta alifunga bao moja kwenye mechi hiyo na kufikisha mabao saba yaliyomfanya kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo.

Samatta aliyezaliwa Januari 7, 1992 anacheza kama mshambuliaji kwenye klabu hiyo yenye makazi yake mjini Lubumbashi.

Mchezaji huyo anajulikana kutokana na magoli saba aliyofunga kwenye mashindano ya klabu bingwa ya CAF. Mwaka huu umekuwa mzuri zaidi kwake kwani ndiye aliyeoongoza kwa kuwa mfungaji bora.

Kulingana na rekodi za Tanzania, Samatta anakuwa mchezaji wa kwanza kuwa mfungaji bora akifuatiwa na mwenziye Thomas Ulimwengu. Kutokana na ushindi huo, TP Mazembe watakwenda kucheza fainali za klabu bingwa ya dunia nchini Japan, Disemba mwaka huu.

Wataungana na timu kutoka Ulaya ambazo ni pamoja na Barcelona na Copa Liberadore, na Timu nyingine kutoka bara la Amerika, Auckland City na Club Amerika.

Kutoka Bara la Asia kuna Al-ahli au Guangzhou Evergrande Taobao wanaweza kuuungana na timu nane kwenye fainali hiyo.

Tukirejea kwa Samatta ambaye anaiwakilisha vyema bendera ya Tanzania, kocha wa TP Mazembe, amesema mchezaji huyo ana nidhamu ya hali ya juu sana.

Wamefurahishwa naye tokea ameingia kwenye timu hiyo na hajawahi kupata kashfa yoyote ya kinidhamu au fujo. Pamoja na hayo Mbwana anakuwa mfungaji bora wa timu hiyo na barani Afrika kwa kufunga magoli mengi. Ni mchezaji anayejituma sana na mwenye juhudi kubwa awapo uwanjani.

Wachezaji na mashabiki wa timu hiyo wanataka wachezaji wazuri kama Samatta kutoka Tanzania waende huko wakawafurahishe zaidi.

Tunamtakia Samatta mafaniko makubwa zaidi katika soka la dunia ili aendelee kuipeperusha bendera.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents