Michezo

Samatta kama Ronaldo, Instagram ya Aston Villa yashuka Followers ghafla

Baadhi ya mashabiki wa soka wameamua ku-Unfollow mtandao wa Instagram wa Aston Villa ghafla huku wengine wakiendelea kufanya hivyo kadiri muda unavyozidi kwenda.

Kitendo hicho cha mashabiki kujiondoa katika mtandao huo wa kijamii wa Aston Villa kimekuja mara tu baada ya Mshambuliaji wa Tanzania Mbwana Samatta kutangazwa kujiunga na klabu ya Fenerbahce ya nchini Uturuki.

Idadi ya wafuasi wa Instagram ya Aston Villa ilikuwa 915K hii ni kabla ya klabu hiyo kuweka wazi kuondoka kwa nyota huyo.

Lakini mara baada ya kutangaza rasmi kuwa Samatta amejiunga na Fenerbahce na wanamtakia kila lakheri Idadi ya wafuasi (followers) ndipo ikaanza kushuka hadi kufikia 911K.

Mpaka sasa naanda habari hii na kukuletea kwako wewe msomaji tayari Folowers wa Instagram wa Aston Villa wameshuka hadi kufikia 909K.

Kitendo kama hiki cha wafuasi kushuka katika klabu pindi mchezaji fulani anapoondoka au kuuzwa kilishawahi kutokea kwa Mchezaji bora kabisa duniani Cristiano Ronaldo alipotoka Real Madrid na kujiunga na Juventus.

Juventus ilifanikiwa kupata wafuasi (followers) milioni 4.7 baada ya kumsajili Cristiano Ronaldo wakati ndani ya saa 24 pekee Real Madrid iliwapoteza milioni 1.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents