Tupo Nawe

Samatta ni habari nyingine kwenye taifa linaloshika nafasi ya kwanza kisoka kwa viwango vya FIFA, kiatu cha dhahabu cha nukia upande wake

Mshambuliaji wa Tanzania na klabu ya KRC Genk, Mbwana Samatta anazidi kuwakimbiza nyota wengine wa ligi kuu ya Ubelgiji maarufu kama division A league, baada ya hapo jana kufikisha goli lake la 20.

Samatta Mbwana Ally forward of Krc Genk – Malinovskyi Ruslan midfielder of Krc Genk – Bailey Leon of Krc Genk during the Jupiler Pro League match between KRC Genk and Club Brugge in Genk, Belgium. *** GENK, BELGIUM – 28/02/2016 Photo by Vincent Kalut / Photo News *** (Photo by William Van Hecke/Corbis via Getty Images)

KRC Genk ikiwa ugenini hapo jana ilikubali kipigo cha mabao 3 – 1 dhidi ya wenyeji wao Club Brugge huku bao pekee la Genk likifungwa na Samatta dakika ya 77 za mchezo.

Samatta mpaka sasa amefunga jumla ya mabao hayo 20 yanayomfanya kuwa kwenye nafasi nzuri ya kuwania kiatu cha dhahabu na kuongoza kwenye msimamo wa ligi hiyo ambayo ipo kwenye nchi ya inayoshika nafasi ya kwanza katika viwango vya ubora wa mchezo wa soka duniani vinavyotolewa na FIFA.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW