DStv Inogilee!

Samatta uso kwa uso na Okwi Jumamosi

Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inatarajia kushuka dimbani Jumamosi hii ya Septemba 8 kuikabili Uganda ‘The Cranes’ mchezo wa kutafuta tiketi ya kufuzu michuano ya Afcon.

Stars itashuka kwenye uwanja wa Mandela uliyopo Namboole nchini Uganda huku ikiongozwa na nahodha wake, Mbwana Samatta anayecheza katika klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji huku upande wa The Cranes, ikiwa chini ya mshambuliaji wake hatari, Emmanuel Okwi anayekipiga kwenye timu ya Simba inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara.

Nahodha wa taifa stars, Mbwana Samatta

Kutokana na mchezo huo kupewa uzito wa hali ya juu hasa kutokana na timu hizi kutoka ukanda mmoja wa Afrika Mashariki wachambuzi wa soka wanapendekeza Stars kuona ikitumia mfumo wa 4-5-1 pale inapo utawala mpira na kubadilika 5-3-2 wakati wa kushambulia kwa kuwa Uganda imekuwa bora zaidi kwenye mfumo wa 4-2-3-1 ambao walitumia hata dhidi ya Misri.

Nahodha wa Uganda ‘The Cranes’, Emmanuel Okwi

Kwa mujibu wa viwango vinavyotolewa na Shirikisho la soka duniani (FIFA) timu ya taifa ya Uganda inashika nafasi ya 82 huku Tanzania ikiwa ya 140.

Timu ya taifa ya Tanzania itawategemea zaidi nyota wake wanaocheza ughaibuni, Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu, Chilunda na Msuva.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW