Habari

Samia Suluhu: Kila Jumamosi ya pili ya mwezi iwe siku ya mazoezi

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi. Samia Suluhu Hassan ametangaza kuitenga kila Jumamosi ya pili ya mwezi kama siku ya kufanya mazoezi nchini.

Bi. Samia ametoa agizo hilo baada ya kushiriki matembezi na kuzindua wa kampeni ya Kitaifa ya kudhibiti Magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwenye viwanja wa Leaders Club jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

“Nitamke kuwa kila Jumamosi ya pili ya mwezi itakuwa siku ya mazoezi kwa afya kwa sababu mazoezi ni afya na nawaasa wananchi kufanya mazoezi na kuanzisha na kujiunga na vikundi vya mazoezi na serikali itatimiza wajibu wake wa kuweka mazingira mazuri ya kufanyia mazoezi kote nchini,” alisema Bi Samia.

Makamu wa Rais pia ameagiza watendaji wa Wizara ya elimu, Sayansi na Teknolojia kurudisha mchaka mchaka mashuleni kulingana na maeneo yalivyo huku akisema mchakamchaka utasaidia kuimarisha afya za wanafunzi na kukabiliana na magonjwa mbalimbali.

“Natoa rai utaratibu wa mchakamchaka katika shule zetu urudishwe mara moja katika muda ambao utaonekana ni muafaka kwa shule husika,” aliongeza.

Pia alitoa muda wa miezi mitatu kwa halmashauri zote nchini kurudisha serikalini haraka maeneo ya michezo yaliyovamiwa na watu kwa ajili ya kufanya shughuli zao binafsi.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents