Technology

Samsung wazindua matoleo manne mapya ya Galaxy S10, yamekuja na sifa za kipekee duniani

Kampuni ya Samsung jana Februari 20, 2019 imetangaza matoleo yake mapya ya S10, S10+, S10e, S10 5G na Samsung Galax Fold, matoleo ambayo yamekuja na sifa mbalimbali za kisasa zaidi.

Galaxy S10 imekuja na teknolojia mpya pamoja na muonekano wa kipekee kabisa. Simu hii inakuja na kioo cha inchi 6.1 chenye resolution ya 1440 x 3040 pixels pamoja na teknolojia ya Dynamic AMOLED.

Samsung Galaxy S10
Galaxy S10

Kamera ya mbele kwa ajili ya Selfie ina Megapixel 10 na uwezo wa kuchukua video zenye ubora wa 2k.

Galaxy S10 inakuja pia na kamera tatu za nyuma, mbili zikiwa na Megapixel 12 na moja ikiwa na Megapixel 16 ambayo hii ni Ultra Wide.

Mbali na kamera, Simu hii ya Galaxy S10 inaendeshwa na processor ya Exynos 9820 Octa (8 nm) – EMEA au Qualcomm SDM855, Snapdragon 855 (7 nm), hii ni kwa simu zitakazo kuwa zinapatikana nchini China, Canada na Marekani.

Processor hizi zinasaidiwa RAM ya GB 8 pamoja na ukubwa wa ndani au ROM ya GB 512 au GB 128, ukubwa unaweza kuongezwa kwa kutumia memory card hadi ya GB 512.

Vilevile Galaxy S10 inakuja na teknolojia mpya ya fingerprint iliyopo chini ya kioo pamoja na teknolojia mpya ya Wireless PowerShare, Teknolojia inayo ruhusu simu hiyo kuchaji simu au vifaa vingine kwa kutumia teknolojia ya wireless kwa kuweka kifaa unachotaka kuchaji nyuma ya simu hiyo.

S10 pia inakuja na betri ya Li-Ion yenye uwezo wa 3,400 mAh yenye uwezo wa kudumu na chaji kwa masaa 24 kutokana na matumizi yako. Betri hii inawezeshwa na teknolojia ya Fast battery charging 15W, yenye uwezo wa kuchaji simu hii hadi asilimia 50 kwa muda wa nusu saa.

Kwa upande wa Galaxy S10 Plus, simu hii inakuja na uwezo mkubwa kuliko simu zote za S10 zilizo zinduliwa hapo jana, ikiwa na uwezo wa mara mbili ya S10.

Samsung Galaxy S10+
S10 Plus

Kamera za Galaxy S10 Plus, simu hii inakuja na kamera mbili kwa mbele zikiwa na Megapixel 10 na nyingine ikiwa na Megapixel 8. Kamera hizo ziko chini ya kioo cha inchi 6.4 chenye resolution ya 1440 x 3040 pixels pamoja na teknolojia ya Dynamic AMOLED.

Sifa nyingine za kipekee, Kwa nyuma Galaxy S10 Plus inakuja na kamera tatu za Megapixel 12 zikiwa mbili na moja ikiwa na Megapixel 16 kama ilivyo Galaxy S10.

Mbali na kamera Galaxy S10 Plus inakuja na processor ya Exynos 9820 Octa (8 nm) – EMEA au Qualcomm SDM855 Snapdragon 855 (7 nm) kwa nchi za China na Marekani. Processor hizi zinasaidiwa na RAM ya GB 12 au GB 8, pamoja na ukubwa wa ndani au ROM ya TB 1 au GB 512. Vilevile unaweza kuongeza ukubwa huo kwa kutumia memory card hadi ya GB 512.

Galaxy S10 Plus inakuja pia na battery kubwa ya Li-Ion yenye uwezo wa 4100 mAh ikiwa na uwezo wa kudumu siku mbili kulingana na matumizi yako.

Sifa nyingine ukiondoa hizo hapo juu, zinafanana na Samsung Galaxy S10 unaweza ukarejea hapo juu.

Simu hii inauzwa kwa Tsh milioni 2.7 bei hii bila makato ya kodi, imepishana kidogo na S10 inayouzwa Tsh Milioni 2.5 .

Samsung Galaxy S10 5G
S10 5G

Hiyo jana pia, matoleo mengine yaliyotangazwa ni Samsung Galaxy S10 5G na Samsung Galaxy Fold yenye uwezo wa kujikunja, simu hizi zote zinakuja na uwezo wa mtandao wa 5G na ndio simu pekee zenye kasi ya 5g duniani.

Samsung Galaxy Fold
Samsung Galaxy Fold simu yenye uwezo wa kujikunja inauzwa Tsh Milioni 4.3 .

Toleo lingine ni la Samsung Galaxy S10e, hii ndio simu yenye uwezo wa kawaida ukilinganisha na matoleo mengine yaliyotangazwa jana.

Samsung Galaxy S10e

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents