Michezo

Samuel Eto’o aipigia magoti Antalyaspor

Nazi haishindani na jiwe. Hatimaye mshambuliaji Samuel Eto’o ameuomba radhi uongozi wa timu yake ya Antalyaspor inayoshiriki ligi kuu ya nchini Uturuki.

etoo

Mchezaji huyo aliingia kitanzini kwa kusimamishwa kutoichezea timu hiyo kwa muda usiojulikana kutokana na maneno aliyoyaandika kwenye mtandao wake wa Instagram mwezi uliopita yanayodaiwa kuwa ya kibaguzi.

“Perhaps some people do not feel respect for me because I am black,” aliandika Eto’o kwenye mtandao huo. Mwenyekiti wa klabu hiyo ya Antalyaspor, Ali Safak Ozturk amesema kuwa Eto’o ameomba radhi na mwenye moyo mgumu mithili ya jiwe linalokaa majini na haliingii maji ndio anapaswa kutokumsahe.

“We hope he will behave more carefully in the future and make a positive contribution to the team,” amesema Ozturk. Timu hiyo inatarajiwa kucheza na Galatasaray kwenye muendelezo wa ligi kuu ya nchi hiyo Jumapili hii.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents