Habari

Samunge sasa yapata mawasiliano

babu_loliondo_airtel1

[Mchungaji Mstaafu Mwaisapile akipokea zawadi ya simu ya Mkononi kutoka airtel. anayemkabidhi ni meneja wa biashara wa Airtel Mkoa wa Arusha, Paschal Bikomagu. Kulia DC, ngorongoro]

Ikiwa ni muendelezo wa kutimiza ahadi yake ya kuleta mawasiliano nafuu na yenye kuwafikia watanzania wengi zaidi, hasa walioko maeneo ya vijijini hapa nchini, kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Airtel, leo imetangaza kuzidi kupanua mtandao wake kwa kuzindiua huduma ya mawasiliano katika eneo la Samunge na maeneo jirani, wilayani Ngorongoro, mkoani Arusha.

 

Kwa mujibu wa Airtel Tanzania, kuzinduliwa kwa mtandao imara na wenye nguvu umegharimu zaidi ya dola za kimarekani laki moja na nusu hadi ulipomalizika. Uwekezaji huu utawezesha kuleta mawasiliano thabiti kwa watu wa vijiji vya Samunge, Mgongo, Mageri, Yasimdito and Digodigo.

babu_loliondo_airtel2

[Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Bw Elias Wawa Lali (katikati), Diwani wa Kata ya Samunge, Bw Jackson Sandea (kulia), Meneja Biashara wa Airtel mkoa wa Arusha, Paschal Bikomagu]

Akitoa maoni yake juu ya uzinduzi huu wa huduma ya mawasiliano, Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Sam Elangalloor amesema kwamba Airtel imejidhatiti vilivyo katika kutoa huduma bora na nafuu kwa watu wa Samunge, huduma inayoambatana na uwepo wa mtandao madhubuti pamoja na huduma nyingine lukuki ambazo zimekuwa zikipatikana na kufurahiwa na wateja wengine wa Airtel Tanzania nzima.

“Uwepo wetu wetu Samunge na maeneo mengine ya jirani, kwa hakika kutaleta chachu ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wakazi na wageni wa maeneo haya. Kuwaunganisha watu wa Loliondo wakati huu ambapo mahitaji ya mawasiliano ni makubwa, kunadhihirisha dhamira yetu ya kuwa mbele zaidi kwa kila tunalofanya”, alieleza zaidi.

Kwa kipindi cha karibuni, eneo la Samunge limeonyesha kuwepo ongezeko kubwa la wageni wanaotembelea, kutoka Afrika ya Mashariki na Kati, wengi wao wakiwa wanaelekea kupata tiba maarufu ya kikombe cha Mchungaji Mstaafu Ambikile Mwaisapile.

Inakadiriwa ya kwamba idadi ya wageni wanaoingia na kutoka siku inafikia hadi watu 25,000, huku eneo hilo likiwa linakabiliwa na uhaba mkubwa wa kutokuwa na mawasiliano ya simu za mkononi. Kwa kuwepo kwa Airtel sasa hivi, kutawawezesha watu kuweza kupiga na kupokea simu na sms, jutumia huduma nafuu ya internet na pia kuweza kutuma na kupokea fedha kupitia Airtel Money.

Vilevile, kuwepo kwa mtandao wa airtel eneo hilo kutawawezesha wageni mbalimbali ambao wengine hutoka nje ya mipaka ya Tanzania kuweza kunufaika na huduma ya One Network, ambayo inawawezesha kuwasiliana kwa kutumia viwango vya gharama vya nchi wanazotoka.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Isidore Shirima amesema “Sisi, kama serikali, tumefarijika sana kuona juhudi hizi za uongozi na wafanyakazi wa airtel katika kuhakikisha wanafikisha huduma ya mawasilano ya simu za mkononi kwa wana jumuia ya samunge na maeneo jirani. Kuwepo kwa mtandao wa Airtel hapa sit u ya kwamba utaleta manufaa ya kiuchumi, bali pia kutachochea maendeleo ya huduma za kijamii kwa wageni na wenyeji”.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents