DStv Inogilee!

Samwel Etoo aendesha mafunzo ya soka kwa watoto jijini Dar Es Salaam (+Video)

Samwel Etoo aendesha mafunzo ya soka kwa watoto jijini Dar Es Salaam

Mchezaji wa zamani klabu ya FC Barcelona na timu ya taifa ya Cameroon yuko Tanzania kwa ajili ya kufungua ujenzi wa uwanja wa soka linalojulikana kama Fives katika fukwe za jiji la Dar Es Salaam.

Etoo aliwasili Tanzania mnamo siku ya Jumatano kwa lengo hilo lakini leo hii asubuhi ameweza kuendesha zoezi la kuwafundisha watoto wadogo soka katika fukwe za Ramada Hotel jiji humo.

Mbali na kuendesha zoezi hilo lakini pia asubuhi mapema siku ya alhamisi aliweza kuzindua ujenzi wa uwanja huo maeneo ya Ufukwe wa Coco beach jiji Dar Es Salaam ambapo ujezi wa uwanja huo utasimamiwa na kampuni ya Castle lager.

Akishirikiana na mlinda malango wa zamani wa klabu ya Simba na timu ya taifa ya Tanzania Ivo Mpunda Etoo ameshiriki katika Clinic ya watoto katika kituo cha mpira wa miguu cha Ivo Mapunda KMC na timu ya ligi kuu ya KMC katika ufukwe wa bahari katika Hoteli ya Ramada jijini Dar Es Salaam.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW