Burudani

‘Sanaa sio uhuni’ – Snura

Msanii wa Bongo Fleva, Snura ameamua kuwachana watu wanaodai kuwa Sanaa imejaa uhuni kwa kuwazibua masikio kuwa uhuni ni tabia ya mtu na wala hauletwi na Sanaa.

Picha inayohusiana
Snura

Snura amesema Sanaa haileti uhuni hata siku moja kwani wapo watu ambao wanafanya uhuni na bado hawapo kwenye sanaa.

Sanaa ni kazi kama kazi nyingine, haihusiani kabisa na uhuni kwani uhuni ni tabia tuu ya mtu mwenyewe nawashauri  akina Mama wanaowakataza watoto wao kuingia kwenye sanaa wasiwakataze“Amesema Snura kwenye mahojiano yake na East Africa Radio.

Mkali huyo wa Chura ameenda mbali zaidi kwa kutoa mfano kuwa wapo akina Mama ntilie ambao hawapo kabisa kwenye sanaa na bado wanafanya uhuni.

Ukisema Sanaa ni uhuni nakushangaa sana kwani wapo akina Mama Ntilie mtaani ni wahuni sana na hawapo kwenye sanaa“,Amesema Snura.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents