Burudani

Sanaipei adai wasanii wa Kenya wameisahau jamii katika nyimbo zao

Hitmaker wa wimbo ‘Amina’ Sanaipei Tande aka Sana amefunguka juu ya mtindo wa uimbaji wao kama wasanii.

Muimbaji huyo ambaye amerudi kwenye game kwa kishindo huu mwaka baada ya kimya kingi, amedai kuwa kinyume cha matarajio, wengi wao wamesahau kuzungumzia vitu vya msingi katika muktadha wa jamii.

Nilipata nafasi ya kuzungumza naye mawili matatu kuhusu masuala mazima ya mipango na matarajio yake kwenye game, hususan huu mwaka. Alisema kwamba ‘content’ ya nyimbo zao kibao kama wasanii, hawajaweka uzito katika kutoa hamasa na labda kuielimisha jamii kwa kuzungumzia masuala yanayoibuka kwa jamii inayowaangalia kwa macho yote.

“Na kama wasanii ni jukumu letu kuleta mambo kama haya machoni mwa watu, ila kuimba tu bila maana inasaidiaje jamii!, alisema mrembo huyo aliye na sauti ya kumtoa nyoka pangoni.

“Lazima pia tutengeneze miziki ya kuelimisha watu wetu na ‘Simama Imara’ ndio sababu yake. Nina nyingine pia nitaaachia labda May,” aliongeza kusema.

Kuhusu ratiba yake ya sasa ya kuachia nyimbo, amesema itakuwa ni mwendo wa bampa to bampa. Tayari ameachia nyimbo mbili huu mwaka na nyingine nyingi zipo kwenye kapu. Sanaipei amewataka mashabiki wake wote kuwa tayari kupokea kazi mpya kutoka kwake kila baada ya miezi miwili.

Wenzetu wanasema kobe akiinama hutunga sheria na ni kweli hakufanya kosa kuwa kimya. Hilo limeanza kudhihirika kwake. Kwa sasa Sanaipei anashughulikia ujio wa video za nyimbo Amina na Simama imara.

Story by: Ted Agwa
Instagram @ teddybway

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents