Michezo

Sanchez na Ozil bado wapowapo sana tu Arsenal

Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amesema wachezaji wake, Alexis Sanchez na Mesut Ozil wataendelea kusalia katika timu hiyo na kamwe hawatoondoka dirisha la usajili la mwezi Januari.

Meneja huyo wa The Gunners, Wenger amesema hakuna uwezekano wowote kwa wachezaji hao wa kimataifa wa Chile na Ujeruman kuondoka Emirates katika dirisha hili lijalo la usajili kutokana na makubaliano waliyoafikiana toka mwanzo mwa msimu.

Arsene Wenger ameyasema hayo wakati wakielekea katika mchezo wao wa hapo kesho dhidi ya Huddersfield “Huwa sifikirii kama wataondoka lakini kwakuwa bado wapo hapa tutalazimika kuwapatia kila mahitaji muhimu watakayo hitaji kupewa ndani ya klabu.” Amesema Wenger.

“Ndani ya kichwa changu ninachofahamu tutaendelea kuwa nao hadi mwishoni mwa msimu. Hayo nimaamuzi ambayo tumeyafanya tangu mwanzoni mwa msimu vinginevyo kutokee kitu kisichotarajiwa.”

Wakati alipoulizwa kama watasalia kwamuda mrefu zaidi ndani ya klabu hiyo Wenger amesema hawezi kujibu swali hilo leo.

The Gunners enter the fixture at the Emirates sitting fourth in the Premier League table 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents