Habari

Sanduku la kupigia kura ladaiwa kuibiwa

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni (CHADEMA), Salum Mwalimu amedai kuibiwa kwa sanduku la kupigia kura katika Mtaa wa Idrisa Magomeni Jijini Dar es Salaam.

Salum Mwalimu ameyasema hayo leo wakati akizungumza na mubshara na kituo cha runinga cha ITV ambapo alisema kuwa alipigiwa simu na Wakala wake kuwa sanduku limekuja kuibiwa na baadae kurudishwa baada ya dakika 10.

“Nimepigiwa simu na wakala wangu kuwa sanduku lilikuja na kuibwa lakini nikazungumza na msamamizi wa kituo hichi pamoja na Polisi ambae ni msamimizi mkuu wote walikiri kuwa sanduku limeibwa na kwa pamoja wote tulikubaliana kuwa sanduku liliibwa na mtu ambae alikuja na kulipora japo watu walikuwa wamekaa hapa hapa akatokomea nalo”, amesema Salum.

“Baada ya dakika kama 10 hivi sanduku likarudishwa. Sasa kinachonishangaza ni kwamba Polisi na Tume wanasema uchaguzi uendelee.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents