Santi Cazorla atoa tumaini jipya Arsenal

Huenda matumaini ya Santi Cazorla kuaribia kurejea kwenye kikosi cha Arsenal zikawa ni taarifa nzuri kidogo na kuwapa furaha mashabiki wa klabu hiyo japo bado mambo yanaonekana kuwa magumu kwa upande wao msimu huu.

Kiungo huyo kutoka Hispania ameonekana akifanya mazoezi Alhamisi hii majira ya mchana kwenye uwanja wa Emirates kabla ya wa Europa League uliowakutanisha Arsnal na Atletico Madrid.

Cazorla hajaonekana uwanjani tangu Oktoba 2016 alipooumia. Hata hivyo kocha Arsene Wenger alipanga kumuongezea mkataba mchezaji huyo.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW