Tupo Nawe

Santi Solari ajificha kwenye kivuli cha Gareth Bale sare yake na Villarreal ‘Yeye ndiyo sababu’

Kocha wa klabu ya Real Madrid, Santi Solari amesema kuwa majeraha ya mshambuliaji wake Gareth Bale ndiyo sababu kubwa ya timu yake kuuanza mwaka 2019 vibaya kwenye ligi kuu ya La Liga baada ya hapo jana kulazimishwa sare ya mabao 2 – 2 dhidi ya Villarreal.

Image result for santi solari vs Villarreal

Villarreal walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza kupitia kwa mchezaji wake Santi Cazorla lakini Madrid wakifanikiwa kusawazisha kupitia kwa Karim Benzema na Raphael Varane kupachika la pili kisha Cazorla kuisawazishia timu yake na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya 2 – 2.

Image result for santi solari vs Villarreal

Baada ya Bale kutolewa mara kadhaa kufuatia kusumbuliwa na matatizo ya misuli timu hiyo ikashindwa kulinda bao lake la pili ndipo nyota wa zamani wa Arsenal, Cazorla kupata bao la kusawazisha.

“Ushindi ulikuwa tayari upo mikononi mwetu na tulihitaji kushinda mechi hii,” amesema Solari.

Santi Cazorla ameongeza “Lakini walirudi kwenye mchezo na kutoa sare. Tunacheza nyumbani na tunahitaji pointi. Gareth ametukharimu anamatatizo na kusababisha kukosa ‘counter-attacking’ na yeye ndiye amebobea katika hilo.”

Kocha huyo raia wa Argentine amesema kuwa walikuwa na nafasi za wazi ya kuweza kupata bao la tatu hasa kupitia kwa Lucas Vazquez na Marcelo lakini walishindwa kufanya hivyo. .Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW