Habari

Sappy: Producer Mtanzania wa Homeboyz, KE, ametayarisha ‘Badder Than Most’ ya Redsan na Swahili Shakespeare ya Rabbit

Khery Sappy ni producer mwenye umri mdogo anayetokea Mwanza. Alianza kutengeneza beats kwa computer yake nyumbani na mara kadhaa kushiriki katika kutengeneza nyimbo kwenye studio ndogo za Mwanza.

IMG-20130612-WA000
Sappy na Redsan

Miaka miwili iliyopita alienda kusomea masuala ya utayarishaji wa muziki kwenye chuo cha Homeboyz ambako baada ya kumaliza, uwezo wake uliwavutia wamiliki na kuamua kumbakiza kama producer wa studio maarufu ya Homeboyz Production.

530667_436033606454934_1851710880_n
Sappy na Prezzo

Jina lake jijini Nairobi ni kubwa mno kwa sasa na ameshafanya kazi na wanamuziki wakubwa wa nchini Kenya. Kazi ya hivi karibuni aliyoifanya ni Badder Than Most ya Redsan ambayo ameiambia Bongo5 kuwa ameshafanya remix ya wimbo huo ambapo ameongezeka msanii wa Jamaica, Demarco aliyekuwa na show jijini Nairobi hivi karibuni. Remix hiyo inatarajiwa kutoka kesho, June 13.

http://www.youtube.com/watch?v=qQQP_8Mz4t4

“Nashukuru Mungu nimepata experience kubwa sana kufanya kazi na international artist, coz Demarco ni producer pia but amerespect kazi yangu,” amesema Sappy.

“Sina uoga wowote wa kufanya kazi na msanii yeyote,”ameongeza.

546890_439009106157384_1768936655_n
Bamboo, Sappy na STL

Sappy amesema ametayarisha albam yote ya Redsan, ngoma mpya ya Prezzo iitwayo Life Celebration itakayotoka Ijumaa hii na Abbas ft Bamboo na Prezzo Tokelezea remix.

Zingine ni wimbo wa Ally B aliomshirikisha Size 8 ‘Silali’ na wimbo wa Rabbit – Swahili Shakespeare. Ameongeza kuwa yupo jikoni pia kufanya wimbo mpya wa Naziz.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents